Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, inatarajia kuanza kutoa hati ya umiliki wa ardhi ndani ya siku moja katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. William Lukuvi katika warsha na waandishi wa habari iliyofanyika jijini Dar es salaam, amesema kuwa lengo la kupanga kutoa hati hiyo ya umiliki wa ardhi  ndani ya siku moja ni kuhakikisha kila mwenye ardhi anamiliki ardhi hiyo kihalali.

“Tungependa kila mwenye kipande cha ardhi apewe hati, nyaraka salama ili amiliki mwenyewe, kama ni eneo la nyumba lipewe hati, hakuna eneo lisilo na mwenyewe, lengo ni kila kipande cha ardhi kipimwe ili mmiliki amiliki halali”amesema Lukuvi.

Hata hivyo amesema kuwa changamoto kubwa waliyonayo kwa sasa hivi ni uwepo wa kiasi kidogo cha ardhi iliyopimwa na kutolewa hati.

Madawa ya kulevya yamwathiri aliyekuwa mshiriki wa BBA Nando
Chadema: Tumejipanga kuchagua viongozi makini