Maafande wa jeshi la kujenga taifa Ruvu Shooting, wataanza msimu mpya wa ligi kuu ya soka Tanzania bara mwishoni mwa juma hili kwa kuwakosa washambuliaji Fully Maganga na Issa Kanduru, ambao ni majeruhi.

Wachezaji hao walipata majeraha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ndanda FC ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja mwishoni mwa juma lililopita kwenye uwanja wa Azam Complex.

Hali ya kukosekana kwa wachezaji hao wawili imezua hofu katika kambi ya Ruvu Shooting ambayo kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya mwisho, kabla ya kuwakabili mabingwa wa Ngao Ya Jamii Wekundu wa Msimbazi Simba.

Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Abdul Mutiki amesema hatua ya kuwakosa wachezaji hao ni pengo kubwa katika safu yake ya ushambuliaji, ambayo pia, itamkosa Abdulrahman Mussa ambaye yupo kwenye timu ya jeshi huko mjini Bujumbura nchini Burundi.

Neymar kutinga mahakamani kupinga madai ya Barcelona
Liverpool yazima ndoto za Hoffenheim kucheza UEFA