Mara baada ya baadhi ya picha kusambaa mtandaoni kuhusu msanii wa muziki Tanzania, Ambwene Yessaya maarufu kama AY, zikionesha amefunga ndoa na mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Remmy.

Taarifa kutoka Rwanda zinasema kwamba sherehe hiyo ilikuwa maalumu kwa ajili ya AY kumtolea mahali mwanadada huyo na sio ndoa kama ilivyodhaniwa na kutafsiriwa na watu wengi wakiwemo baadhi ya wasanii waliotuma pongezi za ndoa hiyo.

Aidha inasemekana kuwa kwa mila na desturi  za Rwanda sherehe ya kutoa mahali hufanyika nyumbani kwa mwanamke, ila siku hiyo AY, alifanya sherehe hiyo katika Hotel ya Golden Tulip La Palisse iliyoko nje kidogo ya mji wa kigali na wazazi wa wapenzi hao walikutana.

Hata hivyo zoezi la utoaji mahali limeambatana na utambulisho wa mwanaume kwa wazazi wa mwanamke.

Sherehe hiyo alihudhuriwa na watu maarufu akiwemo Sallam SK ambaye ni meneja wa AY, Mwana FA na Mtangazaji  B Dozen.

Kupitia mitandao ya kijamii wasanii wa Tanzania wametumia kurasa zao kumpongeza  msanii huyo katika hatua hiyo kubwa ya kimaisha.

Diamond Platinumz ameandika hivi ‘Super Congrats Legend …Mwenyezi Mungu awajalie ndoa yenye furaha, amani na baraka tele @aytanzania”.

Mwana FA naye katika kurasa wake ameandika ”my brother @aytanzania, karibu kwenye hili timu la watu wazima wenzio..Mungu awabariki wewe na shemeji wa Taifa @remyrwanda kwenye muunganiko wenu huu..Godspeed my G. Ila Rwanda hapana aisee”.

Lowassa atoa neno zito kwa Serikali
NEC yafanya mabadiliko msimu huu wa uchaguzi

Comments

comments