Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewaonya watu wanaopanga kufanya maandamano nchi nzima bila kibali cha jeshi hilo.

IGP Sirro ameyasema hayo jana katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Simiyu, ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo.

“Kuna makundi ya vijana wanajiita wanamapinduzi, wanahamasishana kufanya maandamano nchi nzima wakiratibiwa na chama kimoja cha siasa, tumeijipanga kuwadhibiti na tuatawakamata wote bila kujali vyeo vyao,” IGP Sirro anakaririwa.

Aidha, jana Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa aliwataka wazazi kuwaeleza watoto wao kujiepusha na kujihusisha na uchochezi unaoendelea. Aliwataka wananchi kuepuka uchochezi unaofanywa na watu ambao ‘wao wako katika maeneo salama’.

Kamanda Mambosasa alisema Jeshi la polisi litawachukulia hatua wote watakaojihusisha na maandamano au vitendo vyote vinavyohusu uchochezi.

Jeshi na Polisi watofautiana nchini Nigeria
Botswana yamlaumu Kabila kwa ghasia zinazoendelea DRC