Beki kutoka nchini Ublegiji Jan Bert Lieve Vertonghen amesema anatarajia kusaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Tottenham , ambao utaendelea kumuweka kaskazini mwa jijini London hadi mwaka 2020.

Mkataba wa sasa wa beki huyo wa kati, ulisainiwa Disemba 2016 na unatarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu wa 2018/19.

Vertonghen amekua na kiwango kizuri tangu alipojiunga na Spurs mwaka 2012 akitokea Ajax Amsterdam, na amekua sehemu ya kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kwa kipindi kirefu.

“Mkataba wangu utafikia kikono mwishoni mwa msimu huu, lakini uongozi wa Tottenham upo katika mazungumzo ya kutaka kuniongeza mkataba mwingine wa mwaka mmoja,” alisema beki huyo alipohojiwa na vyombo vya habari vya Ubelgiji.

“Nafikiri wameona juhudi zangu kila nichezapo katika michezo ya ligi ya ndani na nje ya England, binafsi nipo tayari kuendelea kuitumikia Spurs mpaka tutakapofikia lengo linalokusudiwa.”

Vertonghen alikuwa sehemu ya kikosi cha Ubelgiji kilichofika hatua ya nusu fainali wakati wa fainali za kombe la dunia nchini Urusi, na anatarajiwa kucheza mpambano wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Scotland kesho Ijumaa.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 31, tayari ameshaitumikia Spurs katika michezo 250, katika michuano yote waliyoshiriki tangu mwaka 2012.

LIVE: Rais Magufuli akihutubia wananchi wilayani Serengeti mkoa wa Mara
Video: DC Katambi amsweka ndani aliyetaka kuvuruga mkutano wake na wananchi

Comments

comments