Rapa kutoka Marekani JAY-Z  ameonekana kuthibitisha kuwa mama yake ni mpenzi wa jinsia moja, katika wimbo uliopo kwenye albamu ya 4:44 JAY-Z kuna mistari inayosema;Mama alikuwa na watoto wanne lakini ni mpenzi wa jinsia moja licha ya kujifanya kuwa muigizaji.

Katika wimbo huo imesikika sauti ya mama yake JAY-Z kwenye (autro) maneno ya mwishi wa wimbo akisema ”Dunia inabadilika na wanasema ni wakati wa kuwa huru/lakini unaishi na hofu ya kuwa wewe mwenyewe”

”Kuishi katika kivuli kunaonekana kuwa eneo salama kuwa, hakuna mtu wa kukushambulia /lakini maisha ni mafupi na ni wakati wa kuwa huru”.

JAY-Z ambaye albamu yake ya 4:44 amekuwa miongoni mwa albamu zinazofanya vizuri sokononi kwa sasa hajawahi kuweka wazi kuhusu mama yakeGloria Carter  juu ya kuwa na mapenzi ya jinsia moja katika nyimbo zake.

Marekani yasema itatumia jeshi kuikomesha Korea Kaskazini, yafyatua mabomu
Video: Manji yamkuta ya vigogo wa Escrow, IGP Sirro: sasa ubaya ubaya tu