Mara baada ya mwimbaji maarufu toka nchini Marekani Rihanna kuipiga chini ofa ya kutumbuiza kwenye fainali ya Super Bowl  kwa kumuunga mkono Colin Kaepernick na kampeni yake ya kupiga goti kupinga uonevu wa mtu mweusi, Jermaine Dupri ameibuka na  kupingana na mtazamo huo

Akizungumza na TMZ  mtayarishaji huyo mkongwe wa muziki  amesema kuwa wasanii wanaozipiga chini ofa za kutumbuiza kwenye Super Bowl  wanakosea sana.

Aidha amesema kuwa kugoma kuandamana hadharani haoni kama ni njia sahihi anafikiri ni bora  wasanii waitumie nafasi hiyo kama  njia ya kufikisha ujumbe wakati wakiwa jukwaani na waichukue fursa hiyo kama faida

“Boycott and marches don’t seem like they work  to me Im sorry I think they should send a message while they on stage take advantage of your platform Alisema mkongwe huyo”

Mwaka jana Jay-Z pia aligoma kutumbuiza kwenye fainali hizo mwaka huu Rihanna ameripotiwa  kuipiga chini ofa hiyo akipinga msimamo wa FNL juu ya kampeni ya Kaepernick.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 1, 2018
Mbaroni kwa kutaka kumpa rushwa polisi

Comments

comments