Meneja wa Man Utd Jose Mourinho amemtaka mshambuliaji wa pembeni wa klabu hiyo Anthony Martial kufuta wazo la kuondoka Old Trafford katika kipindi hiki, na badala yake ajenge fikra za kupambania nafasi katika kikosi cha kwanza.

Mourinho amempasha habari hizo Martial, wakiwa nchini Marekani ambapo kikosi cha Man Utd kimeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi ambao utaanza rasmi August 11.

Wakala wa Martial ambaye ni Philippe Lamboley, mwezi uliopita aliwasilisha ombi la mchezaji wake mwenye umri wa miaka 22 kutaka kuondoka Man Utd, kufuatia kuchoshwa na hatua ya kuwekwa benchi, pamoja na kushindwa kuafikiana na uongozi kuhusu mpakata mpya.

Klabu za Tottenham, Chelsea na Bayern Munich zilitajwa kuwa katika harakati za kumsajili mchezaji huyo kutoka nchini Ufaransa, ambaye alijiunga na Man Utd mwaka 2015 akitokea AS Monaco kwa ada ya Pauni milioni 36.

‘Ninamtaka aweke mawazo yake hapa Los Angeles, ili afanikishe lengo lake la kucheza kwenye kikosi cha kwanza,’ alisema Mourinho.

‘Haiwezekani kuhitaji kufanya jambo kwa maslahi binafsi katika maisha yako, bado ninamuhitaji, anatakiwa kudhihirisha uwezo wake hadi afikie kiwango cha kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

Hata hivyo Martial atamaliza mkataba wa kuitumikia klabu ya Man Utd mwishoni mwa msimu huu, na kama ataendelea kuwepo klabuni hapo pasi na kuuzwa katika kipindi hiki ama mwezi Januari mwakani, ataondoka kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.

Katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo alfajiri kwa saa za Afrika mashariki, Matial alikua sehemu ya kikosi cha Man Utd kilichoshindwa kuwika mbele ya San Jose Earthquakes na kualazimishwa matokeo ya sare ya bila kufungana.

Watano wahukumiwa kunyongwa kesi ya Msuya
Clement Sanga ajiuzulu Young Africans

Comments

comments