Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amepiga marufuku kwa wanafunzi watakaopata mimba kuendelea na masomo na kusema kuwa kufanya hivyo atakuwa amesaidia pakubwa kulinda heshima ya shule.

Ameyasema hayo jana mkoani Pwani wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha matunda kilichopo chalinze mkoani humo, amesema kuwa wanafunzi watakaopata mimba, iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi hawataendelea na masomo.

“Nasema hivi katika utawala wangu sitaruhusu wanafunzi hao waendelee na masomo, hata hao NGO’s wanaotetea naomba wanisikilize vizuri, narudia tena kwenye utawala wangu hawatohsikia kitu kama hicho,”amesema Rais Dkt. Magufuli.

Hata hivyo, Rais Magufuli amezitaka taasisi mbalimbali zinazotetea haki za wanafunzi zitetee mambo ya msingi ambayo yataliletea tija taifa na kuweza kuinua elimu ya Tanzania kitu ambacho kimekuwa kikipigiwa kelele siku zote.

Video: Ben Pol amaliza utata picha zilizozua gumzo, aachia video ya 'Tatu'
Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma Leo Juni 23, 2017