Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameandika barua ambayo itapelekwa kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kwa ajili ya shukrani kwa kutambua mchango wa taifa hilo kwa Tanzania.

Ameyasema hayo alipokutana na timu ya wataalamu wa matibabu ya moyo kutoka nchini Israel na Marekani Ikulu Jijini Dar es salaam wanaoshirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

“Nimeandika barua ambayo nitakukabidhi balozi, umpelekee Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu inayoeleza namna ninavyokubali utendaji kazi wake, najua hii barua itamfikia ili kuonyesha kazi nzuri mliofanya,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, madaktari hao zaidi ya thelathini wamekuja nchini kwa ajili ya kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto 51 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 9, 2018
Watu 12 wafariki dunia shambulizi la Califonia nchini Marekani