Kikosi cha Kagera Sugar leo kimelazimishwa sare ya bao moja kwa moja na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara kwenye uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Azam FC na kufikisha 34 sawa na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao hata hivyo wana mchezo mmoja mkononi.

Kagera Sugar yenyewe inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi 18 na sasa inajinasua mkiani ikirudi nafasi ya 15 kwa wastani wa mabao tu baada ya kulingana kwa pointi na Njombe Mji FC.

Katika mchezo wa leo, Kagera Sugar walitangulia kupata  bao lililofungwa na beki Eladslaus Mfulebe dakika ya 50, kabla ya Iddi Kipagwile kuisawazishia Azam FC dakika ya 53.

Shinyanga wapunguza mauaji ya vikongwe
Jafo awataka Maafisa utumishi kujitathmini

Comments

comments