Mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara mbili mfululizo Meddie Kagere amekanusha taarifa zinazoendelea kusambaa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii, kuhusu mustakabali wake ndani ya kikosi cha mabingwa wa VPL Simba SC.

Kagere amekua anahusishwa na taarifa za kutaka kuihama klabu hiyo na kurejea nyumbani kwao Rwanda kujiunga na APR, kutokana na kuenguliwa kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Sven Vandenbroeck.

Mshambuliaji huyo amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote, na badala yake taendelea kusalia Simba SC kama mkataba wake unavyoeleeza, huku akahidi kuhakiksha anawajibika ipasavyo ili kuiwezesha klabu hiyo kutetea taji la VPL.

“Niko vizuri, sina tatizo lolote na kutopata nafasi ya kucheza sasa inategemea, kwani mazoezi ndio yanampa mchezaji nafasi ya kupangwa kucheza, napambana na naamini siku moja nitarudisha namba yangu, ila niko vizuri, sina tatizo lolote,”

“Nina mkataba na Simba, naipenda Simba kuliko kitu chochote kwa sasa, nasisitiza tena niko sawa na ninaendelea kujifua kwa juhudi ili kusalia kwenye kiwango changu.” Amesema Kagere.

Katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu FC, Kagere alianzia benchi, kabla ya kuingia kipindi cha pili na kufunga bao lililokataliwa na Mwamuzi kwa madai alikua ameotea.

Mambo bado magumu- Lissu
Geita, Kahama kuunganishwa kwa lami