Kamati Kuu ya Utendaji ya TFF imekutana mapema hii leo na kutoa maamuzi ya kuwasimika viongozi wa muda ambao wataziba nafasi zilizoachwa wazi na Rais wa Shirikisho hilo, Jamali Malinzi na Katibu mkuu wake Selestine Mwesigwa.

Aidha, majina yaliyopitishwa ni pamoja na Wallace Karia kuwa Kaimu Rais wa Shirikisho hilo huku Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi kuwa Kaimu Katibu Mkuu.

Hata hivyo, Kamati hiyo imesema kuwa viongozi hao walioteuliwa watakaimu nafasi hizo mpaka pale mahakama itakapotoa maamuzi ya kesi inayowakabili Rais wa Shirikisho hilo, Jamali Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa.

Video: Serikali kuwachukulia hatua kali wanaouibia ushirika
Picha: Messi alivyofunga ndoa ya kifahari na rafiki yake wa utotoni