Bodi la ligi TPL Bodi imefanya mabadiliko ya ratiba ya ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2018/19, ili kutoa nafasi kwa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), ambayo itaweka kambi Afrika kusini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa mzunguuko wa tano wa kundi L, wa kuwania kufuzu fainali za Afrika mwakani, dhidi ya Lesotho.

Michezo iliyofanyiwa mabadiliko ni kati ya African Lyon dhidi ya Young Africans uliokua uchezwe Novemba 7, Azam FC dhidi ya Mbao FC na Simba dhidi ya KMC FC yote ya Novemba 8, mwaka huu mjini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dar es Salaam, afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura amesema kutokana na umuhimu wa timu ya taifa, ndio maana wameamua kusogeza mbele michezo hizo ili kupisha maandalizi hayo.

Amesema kila Mtanzania kwa sasa anataka kuiona Taifa Stars inakata tiketi ya kucheza AFCON, hivyo Bodi ya Ligi imeamamua kuondoa michezo hiyo ili wachezaji waweze kupata muda wa kutosha wa maandalizi katika kambi ya Afrika Kusini.

Katika hatua nyingine Wambura amesema michezo mitatu  ya viporo nayo imepangiwa tarehe, ambazo ni Novemba 21 Young Africans dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Simba SC dhidi ya Lipuli FC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Novemba 22, Azam dhidi ya Ruvu Shootin Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Mazungumzo ya Amani ya Burundi yaanza Tanzania
Serikali yamtaka Wema ajieleze

Comments

comments