Ukiitaja orodha ya wasanii wakubwa Duniani wasio ishiwa namna ya kuifanya jamii imzungumzie kila wakati basi huwezi kuacha kumuweka kwenye namba moja Msanii na Mjariamali maarufu Duniani Kanye Omari West maafuru ‘Ye’, kutokana na namna ambavyo maisha yake yamekuwa na matukio mengi ya kustaajabisha na kufurahisha vile vile. K

Kwa sasa sahau kuhusu mtindo wa yeye kutembea akiwa amevaa maski yenye kuuficha kabisa uso wake, Muda huu Dunia inaujadili mtindo mpya wa nywele wa msanii huyo mwenye heshima kubwa kwenye kiwanda cha muziki wa Dunia.

Mapema octoba 18,2021 majira ya jioni kwa saa za Afrika ya mashariki zilianza kuenea picha Mitandaoni zikumuonyesha ‘Ye’ akiwa katika mizunguko yake ya kila siku huko Chini Marekani huku kichwani akionekana kama mtu aliyenyolewa hovyo hovyo kwa jicho la mtazamaji lakini kiuhalisia hiyo ndio Style mpya ya kunyoa ya msanii huyo, ambaye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Kanye West aliweka picha inayomuonyesha akiwa ameipa kisogo Camera ikiwa ni sehemu ya kuunadi mtindo huo mpya kwa wafuatiliaji wake kote duniani.

Una mtazamo gani kuhusu muendelezo wa matukio ya kanye, hasa katika mfumo wa mtindo wa mavazi na unyoaji ambao amekuwa nao hivi karibuni ?.

Ni wapi alipo  Papii Kocha?'
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 19, 2021