Mbunge wa Kieni Nchini Kenya, Kanini Kega amesema mgombea mwenza wa Urais wa Kenya Rigathi Gachagua hamheshimu Rais wa Nchi hiyo Uhuru Kenyatta, licha ya Rais huyo kumpa kazi kama msaidizi wake binafsi.

Kega amesema, Rigathi alikuwa na kinyongo na Uhuru tangu alipomfuta kazi kama msaidizi wake wa kibinafsi.

Amedai kuwa, Uhuru aliamua kumfuta kazi Gachagua baada ya upotevu wa pesa, akidai kuwa mbunge huyo wa Mathira ndiye aliyehusika na kutoweka kwa pesa hizo katika njia ya kutatanisha.

Matamshi ya Kega, yanajiri baada ya kukosolewa na Viongozi wa Azimio La Umoja ambao tangu wakati huo wamemkashifu Naibu Rais, William Ruto kwa kudokeza kwamba ataunda jopo la majaji kuchunguza kutekwa kwa Serikali iwapo atashinda uchaguzi wa Agosti.

Ruto alisema, iwapo atashinda uchaguzi ujao, serikali yake itaanzisha uchunguzi kuhusu kukamatwa mateka kwa Serikali ndani ya siku 30 na kuhusu kutoweka na ukiukaji wa haki za binadamu.

“Hatuna shida na Uhuru Kenyatta, tunamheshimu na hakuna mtu atakayeingilia kustaafu kwake. Lakini ninamwomba Rais, kwa heshima inayostahili, aniruhusu nikabiliane na Raila Odinga kwa sababu sishindani naye. Uhuru Kenyatta, tafadhali, nipe nafasi nishindane na Odinga,” Ruto alisema.

Mfaume Mfaume: Nilifanya mzoezi kwa miezi mitatu
Yusuph Mhilu azigonganisha Kagera Sugar, Singida Big Stars