Kikosi cha klabu ya Simba kimewasili salama Jijini Mwanza kwa ajili ya kibarua cha mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa dhidi ya Mbao FC Alhamis ya wiki hii.

Jumla ya wachezaji 20 wamesafiri na kikosi huku kadhaa wakisalia Dar es Salaam katika kikosi cha pili kwa ajili kuendelea kujifua kwa mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

Aidha, wachezaji 20 ambao wametua Jijini Mwanza ni walinda mlango, Aishi Manula na Deo Munishi (Dida), Shomary Kapombe, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, Pascal Wawa na Jonas Mkude.

Wengine ni Clatous Chama, James Kotei, Mohammed Ibrahim, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Shiza Kichuya, Meddie Kagere, John Boko, Emanuel Okwi, Mohammed Rashid na Adam Salamba.

Hata hivyo, Simba itakuwa na mzigo wa kusaka alama nyingine tatu baada ya kushindwa kuzipata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Nanda FC huko Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

TTB yaipigia chapuo 787-8 Dreamliner kuanza safari ya India
Video: Major Lazer wampa shavu Burna Boy kwenye ‘All my Life’, kuzuru Afrika

Comments

comments