Hatimaye maneno yamewekwa kando na uhalisia umechukua nafasi yake baada ya kutangazwa rasmi kwa tarehe ya pambano kati ya bingwa wa zamani wa ndondi ambaye hajawahi kushindwa, Floyd Mayweather na bingwa wa UFC, Conor McGregor.

Mayweather amekuwa mtu wa kwanza kuweka wazi kupitia Instagram na Twitter kuwa pambano hilo litafanyika Agosti 26, Las Vegas nchini Marekani.

Pambano hilo ambalo limeandaliwa na kampuni ya Mayweather (Mayweather Promotion) linatarajiwa kuvunja rekodi ya kiwango cha fedha watakachoingiza kwenye pambano moja kati ya wawili hao.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Mayweather kupanda ulingoni baada ya kutangaza kustaafu miaka miwili iliyopita.

Hata hivyo, pambano hilo limekosolewa na baadhi ya mashabiki wa ndondi ambao wamedai kuwa kama Mayweather angetaka kurejea kwenye ulimwengu wa ndondi angekubali pambano la marudiano kati yake na Mfilipino, Manny Pacquiao.

Mzee Akilimali: Clement Sanga Akijiuzulu, Nitafanya Usajili
Godzilla amvaa Nikki Mbishi, ‘nitamrudisha...'

Comments

comments