Licha ya kupoteza mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar Disemba 11 katika uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro, kikosi cha Timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC kesho kitashuka dimbani tena kumenyana na Timu ya Simba katika uwanja wa Makapa Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao KMC FC itakuwa ugenini, utapigwa saa 1.00 jioni na kwamba kikosi hicho cha wana Kino Boys kimejipanga vizuri kuhakikisha kwamba kipotayari kwa mtanange huo na kupata ushindi dhidi ya Simba.

Kikosi hicho ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na Kocha Msaidizi Habibu Kondo hakina hofu katika mchezo huo kwani zaidi kinaangalia namna gani kinaweza kupata alama tatu na hivyo kuendelea kujiimarisha zaidi katika msimamo wa ligi kuu Soka Tanzania Bara.

“Hatuna hofu na mchezo wa kesho kwa sababu tumejipanga vizuri, tunakikosi imara, wachezaji ni wazuri ambao wanaweza kukutana na Timu yoyote na tukapata matokeo, kwa hiyo tumesha waanda wachezaji wetu kwamba mechi ya kesho ipo ndani ya uwezo wetu kikubwa ni kuhakikisha kwamba tunapata alama tatu ambazo ni muhimu.

“Tunafahamu kwamba wametoka kupata ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Mbeya City, lakini hiyo haimaanishi kwamba wakikutana na KMC FC pia watapata matokeo, kwetu wakija wajiandae kisaikolojia kuwa watafungwa.

Hata hivyo katika misimu miwili ya Ligi Kuu iliyopita, KMC FC iliweza kupoteza michezo yake yote ya nyumbani na ugenini huku ikipata matokeo ya ushindi kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Chamazi.

Hivyo kulingana na rekodi hiyo, Kikosi hicho katika msimu huu wa 2020/2021 kimejipanga kuvunja rekodi hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba hakuna mchezo ambao utapotea na badala yake tutakwenda kuibuka na ushindi hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi ilikushuhudia Pira Spana, Pira Kodi, Pira mapato litakalochezwa mbele ya mashabiki zao.

Imetolewa na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya KMC FC

Mabadiliko EU chachu ya ushirikiano baina ya nchi za OACPS
Stephen Sey amvutia Lwandamina