Lady Jay Dee ameendelea kuwachanganya mashabiki wa muziki na wafuatiliaji wa mitandao ya kijamii hususan Instagram, akitumia msemo wake I don’t care (sijali).

Awali, mwimbaji huyo alizua gumzo kubwa baada ya kubadili jina lake (handle) kwenye Instagram akiandika ‘I don’t care’, wakati ambao watu wengi walimvaa wakitaka ahudhurie msiba wa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ambaye alikuwa na uhasama naye wa muda mrefu.

Hivyo, wengi waliamini neno hilo lilikuwa ni ujumbe maalum kuhusu shinikizo hilo.

Lakini hivi sasa Jide ni kama amewabadilishia gia angani, au walimuelewa ndivyo sivyo, kwani ‘I don’t care’ imeonekana kuwa ni mradi mpya wa mwimbaji huyo.

Jide ameweka picha mpya kwenye Instagram yake ambayo haina picha yoyote ya zamani isipokuwa mpya zinazohusu ‘I Don’t Care’, na amewaelekeza watu kukaa mkao wa kupata jambo litakalotokea nchini Afrika Kusini kwenye chumba namba 30.

Katika maandishi yake na picha akiwa juu ya neno ‘I Don’t Care’, amewachanganya zaidi watu akielezea kuwa kuna kuchumbiana (engagement), akiweka na picha ya pete.

“Engagement South Africa .Room 30 #Room30idontcare #Jide2019 #IDontCare.” ameandika.

Chumba namba 30, Afrika Kusini, Kunani pale?(Kwa sauti ya Mkoloni). Tusubiri, muda utaongea na yote yataeleweka, kwenye hili sisi tunajali kuhusu ‘I don’t care’ ni wimbo.

McGregor akamatwa kwa kupora simu
Nikki Mbishi aelezea ujumbe ‘tata’ aliopewa na Ruge

Comments

comments