Baada ya kupisha maandalizi ya timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars) kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Zambia, ligi kuu ya soka ya wanawake hatua ya nane bora itaendelea tena mwishoni mwa juma hili kwenye viwanja tofauti.

Hatua ya nane bora inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini mwishoni mwa juma hili itaingia katika mzunguuko wa tano.

Timu shiriki katika ligi hiyo ni Panama FC ya Iringa inayotumia Uwanja wa Samora,Evergreen Queens ya Dar es Salaam inayotumia Uwanja wa Karume na JKT Queens ya Dar es Salaam wanaotumia Uwanja wa Mbweni.

Nyingine ni Alliance ya Mwanza wanaotumia Uwanja wa Nyamagana,Mabingwa watetezi Mlandizi Queens ya Pwani wanaotumia Uwanja wa Mabatini,Baobab ya Dodoma wanaotumia Uwanja wa Jamhuri Dodoma,Kigoma Sisters ya Kigoma wanaotumia Uwanja wa Lake Tanganyika na Simba Queens wanaotumia Uwanja wa Karume.

Huu ni msimu wa pili wa ligi ya Wanawake kuchezwa ambapo katika msimu wake timu ya Mlandizi Queens waliibuka mabingwa.

Katwila ataja sababu za kufungwa dhidi ya Simba SC
Trump achukizwa na kitendo cha FBI kupekua ofisi za Cohen