Lil Wayne ameweka wazi kinachoendelea kati yake na Jay Z, ikiwa ni siku chache baada ya kusikika kwenye tamasha akisema ‘It’s the Roc’, sentensi ambayo ilitafsiriwa na wengi kuwa alimaanisha anajiunga na ‘Roc Nation’ ya nguli huyo.

Kauli hiyo ya Lil Wayne iliibua mengi kutokana na ukweli kuwa ana mgogoro mzito kati yake na bosi wake Birdman na amewahi kutaka kuachana naye akimtuhumu kumkandamiza kifedha na kumrudisha nyuma.

Akifunguka hivi karibuni kwenye kipindi cha Undisputed cha FS1, Lil Wayne alisema kuwa Jay Z ni mtu mwema sana na kwamba amekubaliana naye kuwa atamsaidia tu.

“Jay ni mtu mwema. Hakukuwa na kitu lakini ni rahisi tu kati ya rafiki na rafiki yake, ‘ninataka kukusaidia tu’,” alisema akimkariri Jay Z. “Kirahisi tu, na ndivyo ilivyokuwa, ‘ninataka nikusaidie kadiri niwezavyo’. Hivi sasa atanisaidia, hivyo ndivyo ilivyo,” aliongeza.

Hata hivyo, alikanusha kuwa anapanga kuhamia kwenye ngome ya Roc Nation kama inavyoelezwa na wengi. Alisisitiza kuwa bado wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo lao yeye na bosi wake Birdman akiwa chini ya Cash Money.

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 23, 2017
Vijana Dar watumia ‘mafuriko’ kama fursa mpya