Klabu ya Liverpool imekataa ofa ya usajili wa mkopo iliyotumwa huko Alfield ikimlenga beki wa kati kutoka nchini Ufaransa Mamadou Sakho.

Uongozi wa Southampton ulituma ofa hiyo kwa kuamini huenda Liverpool wangekubali kirahisi kumuachia Sakho, ambaye kwa sasa amekosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Jürgen Klopp.

Liverpool wamefikia maamuzi hayo, kwa kuamini sio wakati sahihi kumuachia Sakho kwa makubaliano ya mkopo, kutokana na hitaji la kutaka kuona beki huyo anaondoka jumla.

Mwanzoni mwa msimu huu, Sakho alikataa kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu za West Brom na Stoke city kwa kuamini alikua na nafasi kubwa ya kuuzwa jumla.

Hata hivyo Southampton bado wana nafasi ya kutuma ofa nyingine itakayo karibia Paundi milion 20, ili kufanikisha usajili wa moja kwa moja wa beki huyo mwenye umri wa miaka 26.

Southampton wameingia sokoni kumsaka mchezaji anaecheza nafasi ya ulinzi, kufuatia beki wao kutoka nchini Ureno José Fonte kuomba kuondoka katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Serikali kuboresha mradi wa maji Makambako
Msipoteze muda kuwaambia sheria inataka nini-Mwijage