Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage, amezitaka Taasisi zilizopo chini ya Wizara yake kutopoteza muda kuwaambia wajasiliamali sheria inasemaje bali wawaonyeshe wafanye nini ili waweze kufanikiwa na si kupoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokutana na mshindi wa Tuzo ya ‘Afrika Enterprenureship Award’ Jennifer Shigoli na kufanaya mazungumzo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Malkia Investment iliyobuni mpango wa kuzalisha taulo za kike ziitwazo ELEA.

Katika mazungumzo hayo Mwijage amempongeza mjasiliamali huyo kwa kuweza kufanikiwa kupata tuzo hiyo ambayo imeliletea Taifa sifa na amemtaka kuongeza juhudi katika shughuli zake.

Aidha, Mwijage amezitaka Taasisi zilizo chini ya Wizara kama Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo (TEMDO) pamoja na Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini (CARMATEC) kuwasaidia na kuwaendeleza Wajasiliamali wadogo ili waweze kusonga mbele.

“Waonyeshe wafanye nini ili wafanikiwe, msipoteze muda kuwaambia sharia inazuia nini” amesema Mwijage.

Kwa upande wake Jennifer, amemshukuru Mwijage kwa kuonyesha nia yakuwa saidia wajasiliamari na ameahidi kuongeza jitihada katika shughuli zake ili kuiwezesha jumuiya ya Watanzania kupata ufumbuzi wa tatizo la taulo za kike kwa Wanawake wa Tanzania.

Liverpool Wagoma Kumuuza Mamadou Sakho
Dani Carvajal Aumia, Kukaa Nje Mwezi Mmoja