Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa takribani saa nne katika ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), kwa kosa la uchochezi.

Mwanasheria wa Chadema aliyeambatana na Lowassa katika ofisi hiyo iliyoko Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ohio jijini Dar es Salaam, Peter Kibatala amesema kuwa mwanasiasa huyo amejidhamini mwenyewe na anatakiwa kurejea katika ofisi hizo Alhamisi saa 6 kamili mchana.

Kibatala amesema kuwa Lowassa ameandika maelezo ya onyo kuhusu kauli aliyoitoa Juni 23 mwaka huu aliposhiriki futari iliyoandaliwa na madiwani wa Chadema.

“Amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23, wakati wa futari iliyoandaliwa na [Mwita] Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika maelezo ya onyo na anatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29,” alisema mwanasheria huyo wa Chadema.

Lowassa anadaiwa kuzungumzia suala la mashekhe wa Jumuiya ya Uamsho waliokamatwa mwaka 2012, akimuomba Rais Magufuli awaachie huru.

Magazeti ya Tanzania leo Juni 28, 2017
Israel yatoa mwaliko kwa Watanzania, yawataka wananchi kutembelea nchi hiyo