Uongozi wa klabu ya Young Africans umetangaza kumtimua kocha wake Luc Eymael baada ya sauti yake yenye ujumbe wa ubaguzi kusambaa katika mitandao ya kijamii, pamoja na vituo mbalimbali vya habari.

Taarifa iliyotolewa mapema hii leo na klabu hiyo imesema kuwa umemfuta kazi leo Julai 27, 2020 na anatakiwa kuondoka nchini haraka iwezekanavyo.

“Klabu ya Yanga unawaomba radhi viongozi wa nchi, Shirikisho la Soka Tanzania, wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga kutokana na kauli za kuudhi na kudhalilisha zilizotolewa na Eymael”

TFF kumpeleka Eymael FIFA
Picha: Uzinduzi wa kanisa la TAG CANA Dodoma