Kiungo kutoka nchini Brazil Lucas Leiva amekamilisha usajili wa kijiunga na wababe wa mjini Roma nchini Italia SS Lazio, akitokea kwa majogoo wa jiji Liverpool.

SS Lazio imeripotiwa kukamilisha usajili wa kiungo huyo, kwa ada ya Pauni milioni 5.

Kiungo huyo alifanyiwa vipimo vya afya mjini Roma mwanzoni mwa juma hili, na usiku wa kuamkia leo alithibitishwa ramsi kuwa mchezaji halali wa SS Lazio.

Baada ya kuthibitishwa kuwa mali ya klabu hiyo, Lucas aliwashukuru wale wote waliofanikisha mafanikio yake ya soka hadi kufikia hatua ya kujiunga na SS Lazio.

“Asanteni sana mashabiki wangu wote popote pale mlipo duniani, nimepitia katika wakati mgumu zaidi, lakini sikukata tamaa hadi kufikia leo ninajiunga na klabu yangu mpya ya SS Lazio.”

“Niliitumikia Liverpool kwa moyo wangu wote, na kwa kiwango nilichokionyesha naamini ilitosha kuondoka Anfield na kuja hapa ili nianze maisha mapya,”

“Ninaishukuru sana familia yangu, mke wangu na watoto wangu kutokana na kipindi chote kuonyesha kuwa na mimi na wamekua wakinipa ushirikiano mzuri ninapokua katika mazingira ya kazi na hata nje ya kazi.”

Lucas mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na Liverpool mwaka 2007 akitokea Gremio ya nchini kwao Brazil, na mpaka anaondoka Anfield alikua amecheza michezo 346 na kushinda taji la kombe la ligi.

JPM atoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya mafuta nchini
Paris Saint-Germain Wajizatiti Kwa Neymar