Msanii wa kundi la Tip Top Connection, Madee amemuomba radhi msanii wa bongo movie, Jacqueline Wolper kwa kutumia taswira ya mrembo huyo kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Sikila’ bila ya ridhaa yake.

Video hiyo ambayo  ipo katika mfumo wa katuni akiwa amemshirikisha Tekno kutoka Nigeria, Madee amekiri kuwa hakumpa taarifa mrembo huyo juu ya kutumia taswira yake katika video hiyo.

Hivi karibuni, Wolper alitumia ukurasa wake wa instagram kuonesha hasira zake juu ya kitendo hicho na kutishia kumstaki Madee kwa  kutumia taswira bila ridhaa yake.

“Niliamua kumtumia Jacqueline Wolper baada ya ‘director’ kuniambia nitafute picha ya msanii yeyote maarufu, ndipo nikaamua kumpatia picha ya Wolper,” Madee ameiambia EATV. Baada ya video kutoka makelele yameanza. So, naomba Jack anisamehe kwasababu kweli sikumpa taarifa,’’ amesema Madee.

“Jack ni rafiki yangu na ataendelea kuwa rafiki yangu na ninamuomba aiangalie vizuri video huenda akaipenda,” ameongeza.

Madee amedai kuwa haamini kama ni kweli mrembo huyo anataka kumfungulia kesi juu ya jambo hilo.

Video: Halmashauri zote zimenyang'anywa mamlaka za kutengeneza barabara-Mdee
Kocha Super Eagles amvuta Enyeama