Magari yanayotumia Nishati ya umeme nchini kenya yameanza kufanya kazi rasimi mapema hii leo yakiwa chini ya uangalizi wa kampuni ya magari ya knights energy inayohamasisha watu kutumia magari hayo ili kukabiliana na onngezeko la joto duniani.

Aidha magari hayo yanauwezo wa kusafiri kilomita 90 mpaka 135 na kusaidia kuondoa tatizo la mafuta ambalo limekua likiwasumbua wananchi, msimamizi wa kampuni hiyo bw, Francis Romano amesema kua wameamua kuleta tekinolojia hiyo ili kukabiliana na ongezeko la joto duniani.

Hata hivyo pamoja na kuingia kwa teknolojia hiyo bw,Romano amebainisha kuwa changamoto  watakazo kumbana nazo ni pamoja na ukosefu wa vituo vya kuchajia magari pindi yanapokua mbali na vituo.

Tusikubali Kuingia Kwenye Uchaguzi Mkuu Bila Katiba Mpya - Mngeja
Kipre Tchetche Akaribia Kuondoka Azam Complex