Takribani magunia 102 ya mchele wa plastiki yenye nembo iliyoandikwa “Best Tomato Rice” yaliyokuwa yanaingizwa nchini Nigeria na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sherehe yamekamatwa.

Taarifa hiyo imetolewa na afisa wa forodha katika mji mkuu Nigeria , Lagos ambapo ameeleza kuwa uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa “plastiki”, baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida

Amesema tukio hilo ni lakustaajabisha sana kwani ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama mchele huo ungeliwa na binadamu.

Afisa huyo amesema kuwa aliwaonya wahujumu uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.

Haarifa zilizopo hadi sasa ni kwamba uchunguzi unaendelea ili kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria.

Shamte ‘Hatihati’ City VS Toto Africans
Busara za Jaji zampa Lema mlango wa kutoka Mahabusu