Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze ahakikishe mpaka kufikia Oktoba 16, 2021 dawa ziwe zimepatikana katika maeneo yote nchini.

Waziri Mkuu amesema kuwa ni maelekezo ya Serikali kuwa vituo vyote vya kutolea huduma zikiwamo zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, hospitali za rufaa za mikoa lazima zipate dawa kwa kuwa zinategemea MSD.

”Nimetoa wiki moja kuanzia jumamosi wiki ijayo, tupate taarifa dawa sasa zinapatikana malori kila zone kumi kumi hakuna zone yenye mikoa kumi zone inamikoa miwili mitatu labda nyanda za juu hayo ni maelekezo ya serikali kwamba tunataka tuone vituo vya huduma vyote zahanati, hospitali za halmashauri, hospitali za wilaya kule kwenye mikoa hospitali za rufaa hizi zote lazima zipate dawa na zinategemea MSD”

”Serikali inapeleka fedha kila mwezi tena tumekubaliana miezi mitatu mitatu na hiyo yote haiendi kwao inakuja kwenu ‘cash’ kwahiyo nyie pale swala la uhasibu na upangaji kwenye bohari, usambazaji ni jukumu lenu kama kuna feli manaake unafeli pale kwako hali hii nimekuta kuanzia kagera, kigoma ,kilimanjaro wapo wananchi wanategemea kituo cha afya lakini hakuna dawa”

Taifa Stars yarejea nyumbani kwa shangwe
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 11, 2021