Uongozi Klabu ya Majimaji FC umetangaza kuwatema wachezaji 16 katika kipindi hiki cha usajili wa msimu wa 2017/18.

Wachezaji waliotemwa ni kipa Agathon Antony, Kutche Bidual, Peter Joseph,Emanuel Semwanza, Paul Nyange, Taria Simba, Said Mrisho na Seleman Kibuta.

Wengine ni Mfanyeje Mussa, George Mpole,Yusuph Mgwao, Adam Siba, Wazir Salum,Bahati Yusuph,Ibrahim Mohamed na Sadat Mohamed.

Katibu Mkuu wa Majimaji, Zakharia Mgalimayo, amesema wachezaji hao wengi ni wale waliomaliza mikataba yao na kwa mujibu wa ripoti ya kocha wa timu hiyo, Kali Ongala,walishindwa kukidhi matarajio.

“Kila tunachokifanya ni kwa mujibu wa ripoti ya kocha, hivyo kuachana na wachezaji hao kunatoa nafasi ya kuwasajili wengine bora zaidi, kwani mipango yetu ni kuhakikisha tunakuwa na kikosi imara cha ushindani msimu ujao, ukizingatia msimu uliopita tuliponea chupuchupu kushuka daraja,” alisema.

Florian Lejeune Kuikamua Newcastle Utd £8.7
FIFA Wainyooshea Kidole Mexico