Waziri wa Nishati, January Makamba mapema leo amekutana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Equinor ya Norway, Bi. Nina Koch jijini Dodoma, ili kuzungumzia maandalizi ya uwekezaji wa mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia (LNG).

Katika mazungumzo yao, Waziri Makamba amesema anaridhishwa na hatua iliyofikiwa na kusisitiza kuwa matarajio yake ya kuona mradi huo ukitekelezwa kwa wakati kama ilivyopangwa ambapo  timu za majadiliano za upande wa Serikali ya Tanzania na wawekezaji zipo katika hatua ya Uandishi (drafting), ya mikataba ya mwisho (final agreements).

Waziri wa Nishati, January Makamba mapema leo amekutana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Equinor ya Norway, Bi. Nina Koch jijini Dodoma.

Kwa upande wake Bi. Koch amesema, ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi Equinor ipo tayari kutoa ushirikiano katika uanzishaji wa Ofisi Maalum ya Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi asilia (LNG Project Office), ambayo itasimamia na kuratibu shughuli za mradi katika kipindi cha ujenzi na uendeshaji.

Bi. Kochi amesema, “kwa uzoefu wangu miradi kama hii, si rahisi kukubalika moja kwa moja na pande zote yaani Kampuni na Uongozi wa Nchi. Lakini kwa mradi huu, uongozi wa kisiasa na wananchi wote wa Norway wanauunga mkono.”

Kikao kikiendelea.

Katika kikao hicho Waziri Makamba aliambatana na Kamishna wa Mafuta na Gesi wa Wizara ya Nishati, Mike Mjinja na Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Charles Sangweni huku upande wa Equinor, akiwepo Bi. Koch aliyengozana na Mkuu wa Kitengo cha Mkondo wa Juu Kimataifa, Nizar Damree.

Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha mkondo wa juu kimataifa, Nizar Damree, Makamu wa Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Equnor Tanzania Bi. Unni Fjaer na Afisa Mawasiliano Equinor Tanzania, Bi. Genevieve Kasanga.

CCM 'yakubali' utendaji wa Serikali Bara na Zanzibar
Geita Gold FC: Hatutasajili kwa Mihemko