Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemshauri Waziri wa Maliasili na Utali, Dk. Hamis Kigwangalla kuchapa kazi na kuachana na mitandao.

Amesema hayo kupitia akaunti yake ya Twetter baada ya waziri huyo kutuhumiwa katika mitandao ya kijamii kuwa ni mwizi nbaada ya ripoti ya CAG kueleza ofisi yake imetumia sh Bilioni 2.58 bila idhini ya bunge

“Kaka yangu unajua ninavyokuthamini chapa kazi achana na mitandao,” ameandika  Makonda

Hata hivyo Waziri Kigwangalla alitoa ufafanuzi kupitia mtandao wa twetter ambaponkuwa yeye sio mwizi na hajawahi kupokea rushwa.

Aidha baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii walimcharua huku wengine wakimuita ni mwizi.

Haji Manara ashindilia msumari Bilioni 20 Simba SC
Molinga asuburi baraka za Young Africans