Klabu ya Man Utd imetaka suala la Ander Herrera kutuhumiwa kuitemea mate nembo ya mahasimu wao Man City, lisikuzwe na kuonekana kama kosa kubwa mbele ya wadau wa soka duniani.

Man Utd imetangaza msimamo huo kupitia idara yake ya habari, baada ya kuona jambo hilo linapewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari, mara baada ya mchezo wao dhidi ya Man City uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Picha za televisheni zilimuonyesha Herrera akitema mate kwenye nembo ya klabu ya Man City iliopo mita chache kutoka eneo la kuchezea.

Kiungo huyo alifanya hivyo wakati wa mapumziko, jambo ambalo limepokelewa kama dharau dhidi ya Man City ambayo ni sehemu ya maendeleo ya soka nchini England.

Kitendo hicho kilionyesha kumkera mmoja wa maafisa wa klabu ya Man City ambaye amedai atalifikisha jambo hilo mbele ya viongozi wa chama cha soka nchini England FA.

Msemami wa klabu ya Man Utd amesema, Herrera hakufanya jambo hilo kwa makusudi na wala hakufahamu sehemu aliekuwepo kuna nembo ya mahasimu wao, hivyo ameomba jambo hilo lichukuliwe kama kosa la kawaida.

“Ander Herrera ameona picha za tukio hilo, na ametueleza wazi hakukusudia kufanya kama inavyofikiriwa na wengi, ametuambia alitema mate kama ilivyo kawaida ya wachezaji wengine wanapokua uwanjani.

“Na kwa upande wetu tumejiridhisha haikuwa jambo la kukusudia, hasa ikizingatiwa nembo ya mahasimu wetu ipo karibu na eneo la kuchezea.”

Katika mchezo huo Man Utd walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri, baada ya kutanguliwa mabao mawili katika kipindi cha kwanza.

Cesar Azpilicueta: Kombe la FA halitoficha udhaifu wetu
Kakobe kuhojiwa Uhamiaji leo