Purukushani za kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Ujerumani, kati ya Manuel Neuer wa FC Bayern Munich na Marc Andre ter Stegen wa FC Barcelona, huenda zikafikia kikomo baada ya fainali za mataifa ya Ulaya 2020 (Euro 2020).

Wawili hao wamekua gumzo la nani anapaswa kuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Ujerumani, kutokana na uwezo na umahiri wanapokua kwenye utetezi wa klabu zao, ambazo zinafanya vyema kwenye ligi za Ujerumani na Hispania.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa leo jumatano kwenye jarida la michezo la SportBild, imeelezwa kuwa, mlinda mlango wa FC Bayern Munich Manuel Neuer, huenda akatangaza kustafu kucheza timu ya taifa baada ya fainali za Euro 2020.

Neuer, ambaye tayari ameshaitumikia timu ya taifa ya Ujerumani katika michezo 90, amekua chaguo la kwanza kwenye kikosi cha mabingwa hao wa dunia mwaka 1954, 1974, 1990 na 2014 tangu mwaka 2010, lakini kwa miaka ya karibuni amekua akipata upinzani mkali kutoka kwa Ter Stegen aliecheza michezo 22 mpaka sasa.

Hata hivyo hatua ya kuanzishwa katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za Euro 2020 dhidi ya Uholanzi na Ireland kaskazini iliochezwa mapema mwezi huu, jarida hilo limeeleza kuwa, Neuer ameonyehsa kujiamini, lakini amedhamiria mwakani atalazimika kustaafu.

Image result for Manuel NeuerManuel Neuer (Kulia) akiwa na Marc Andre ter Stegen (Kushoto) kabla ya moja ya michezo ya timu ya taifa ya Ujerumani.

Jarida hilo limoengeza kuwa, dhumuni kubwa la mlinda mlango huyo mwenye umri 33, ni kutaka kutoa nafasi kwa mpinzani wake Ter Stegen, ambaye bado ana umri mdogo, na inaaminiwa huenda akatumika kwenye kikosi cha Ujerumani kwa kipindi kirefu zaidi.

Neuer, ameendelea kuweka rekodi ya kuwa changuo la kwanza katika kikosi cha FC Bayern Munich pindi kinapocheza michezo ya ligi ya ndani pamoja na ligi ya mabingwa barani Ulaya, huku akiweka historia ya kuwa mlinda mlango aliecheza michezo yote ya fainali za kombe la dunia mwaka 2014, na kutwaa ubingwa

Dhamira yake kubwa aliyoibakisha ni kushiriki michuano ya Euro 2020, na kisha kutangaza kustaafu soka upande wa timu ya taifa, ali ajipe muda mwingi wa kuitumikia klabu yake ya FC Bayern Munich.

Mwenge wa uhuru wakataa mradi wa mamilioni Njombe
Msongo wa Mawazo husababisha kitambi