Baada ya kuitumikia klabu ya Manchester United kwa miaka mitatu, wakala wa mshambuliaji Anthony Martial amethibitisha kuwa mteja wake anataka kuondoka katika klabu hiyo.

Philippe Lamboley amesema kuwa Manchester United wameonyesha nia ya kutaka kuendelea kupata huduma ya mchezaji huyo lakini pande zote mbili zimeshindwa kufikia makubaliano kwa miezi kadhaa sasa.

Matrial amecheza michezo 18 tu ya ligi kuu na kupachika mabao 9 msimu uliomalizika huku akiwa amekosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha United tangu kuwasili kwa Alexis Sanchez mwezi Januari mwaka huu.

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho, amekuwa akimkosoa sana Martial na kumpa nafasi finyu katika kikosi cha kwanza hali ambayo hamridhishi mshambuliaji huyo.

Tangu ajiunge na Man Utd mwaka 2015 akitokea Monaco Martial ameshinda mataji ya EFL cup, FA cup na Europa league.

 

Serikali yatoboa siri elimu bure hadi chuo kikuu
Umuhimu na dhima ya maadhimisho ya siku ya utoaji damu duniani.

Comments

comments