Chama cha soka nchini England (FA) kimeanza kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha vurugu za mashabiki zilizoibuka wakati wa mchezo wa kombe la ligi kati ya West Ham Utd dhidi ya Chelsea, uliochezwa kwenye uwanja wa London usiku wa kuamkia jana.

FA wametangaza kuanza kufanya uchunguzi, huku ikiwa tayari jeshi la polisi linawashikilia mashabiki saba ambao wanadaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.

Mashabiki wa West Ham Utd na Chelsea alionekana kukinzana kwa kauli huku wakirushiana vitu kama sarafu, viti vya kukalia, chupa za vimiminika pamoja na vitu vingine.

Uchunguzi wa FA unatarajia kuegemea sana katika picha zilizorekodiwa na kamera za CCTV zilizofungwa kwenye uwanja wa London.

Yanga Yamgeuka Lwandamina, Yamrudisha Babu Pluijm
Watatu Nje City Vs Majimaji Kesho