Baada ya kufuatilia kesi dhidi ya Bernard Morrison kwa njia ya Mtandao leo Alhamisi (Julai 29), Uongozi wa Young Africans umewataka Mashabiki na Wanachama wao kuwa wastahamilivu.

Young Africans walifungua Mashtaka ya kukata rufaa kwenye Mahakama ya Usuluhushi ‘CAS’ dhidi ya hukumu ya Morrison iliyotangazwa mwanzoni mwa msimu wa 2020/21 na kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.

Kamati hiyo ya TFF ilijiridhisha mkataba uliokuwa unadaiwa upo kisheria baina ya pande hizo una mapungufu, hivyo ilimuweka huru kiungo huyo kutoka Ghana na siku chache alisajiliwa Simba SC.

Taarifa ya Young Africans kwa Wanachama na Mashabiki imeeleza kuwa: Mahakama ya kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) leo imemaliza kulisikiliza kesi ya rufaa ya Klabu ya Yanga dhidi ya Bernard Morrison.

Mara baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo, CAS itatoa uamuzi kwa mujibu wa taratibu zake kuanzia sasa mpaka tarehe 24/08/2021.

Uongozi wa Yanga unawaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki kuwa na subira, wakati huu ambapo Mahakama hiyo inaendelea kukamilisha uamuzi wake.

Morrison afuatilia kesi bila uwoga
Gerson Msigwa akemea upotoshaji unaoendelea mitandaoni