Mwimbaji mkongwe, Matonya ameibuka na madai dhidi ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Diamond Platinumz akidai kuwa wamemuibia kupitia wimbo wake aliouachia miaka kadhaa iliyopita ‘Zilipendwa’.

Matonya amedai kuwa alipaswa kufanya makubaliano na WCB kabla hawajaachia wimbo wao mpya ‘Zilipendwa’ huku akifananisha hatua hiyo na makubaliano yaliyofanywa kati ya lebo hiyo na Saida Kalori walipotaka kutumia wimbo wake ‘Maria Salome’ kuandaa ‘Salome’.

Mwimbaji huyo ameandika ujumbe wake kwa WCB kupitia Instagram akiahidi kutafuta kile alichokiita haki yake.

“Nduguzangu wasafi / Nawapongeza sana kwa kazi mzuri mnazo zifanya / Nilifurahi Sana mlichokifanya kwa saida karoli dadaetu/ mlimuita mkamshirikisha akawapa Baraka zake/ kwangu mlishindwa nini? Sina shida Ya Pesa nina shida Ya heshima cose najua dunia ni mapito/ kama mimi naibiwa haki yangu vipi wasanii wachanga? Basata mkowapi? Wadau Wa muziki mkowapi? Usipo ziba ufa tajenga kuta!! Khaaa tena Bila woga???? lakini haki itafata mkondo wake,” ameandika Matonya.

Jana WCB waliachia ‘Zilipendwa’ ambapo kwa mara ya kwanza wamesikika kwa wingi zaidi kwenye wimbo mmoja. Wimbo huo unafanya vizuri ukitajwa kuwa namba mbili kwenye trending ‘YouTube’.

Nuh Mziwanda azungumzia mpango wa kuacha muziki
Uchambuzi: ‘Seduce Me’ ya Ali Kiba ni ‘Hai au Hoi’?