Vita ya maneno kati ya Ali Kiba na Diamond Platinumz iliyofunika mitandao ya kijamii jana nchini Tanzania imeendelea kukorezwa na ‘watu wa pembeni’, huku maneno aliyotumia King Kiba kumvaa mshindani wake yakivuma kama upepo wa kisulisuli, yaani ‘penseli na unikome’.

Haya ni maneno ambayo aliyatumia Ali Kiba kujibu mualiko wa Diamond kuhudhuria Wasafi Festival, akidai kuwa anachokifanya ni utoto sawa na mwizi aliyemuibia penseli halafu anarudi kutaka kumsaidia kutafuta. Alimtaka ‘Amkome’ au atamuacha uchi.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha ambaye wengi wamemuona kama ni ‘mtu wa pembeni’ jana aliununua ugomvi huo akimvaa Ali Kiba kupitia Instagram, akieleza kuwa kwanza haamini aliyeandika ujumbe wa kumvaa Diamond ni yeye au mkewe.

Mbasha amerusha kombora lake akifahamu kuwa atashambuliwa pia na ‘nyuki’wa timu Kiba. Amendika:

Leo nilikuwa busy kidogo na kazi zangu hivyo sikupata muda wa kuingia mtandaoni ila usiku huu nimeingia na kuona alichokipost Ally Kiba juu ya Diamond nikashangaa sana. Hadi sasa sijajua kama ni Ally Kiba au mke wake ndiyo kaandika hivyo ila kwa kweli nimehuzunika sana. Napenda kutumia muda huu kumkumbusha Ally Kiba kuwa Mungu alimpa nafasi kubwa sana kabla wakati wake haujapita, nadhani yeye ndiyo msanii wa kwanza Tanzania kuimba na msanii mkubwa kama R Kelly ila cha ajabu katika wakati wake hakuweza kujibrand, sasa wenzake wanajibrand na kuutumia wakati wao vizuri yeye anaanza kuwa na uchungu na kuhisi kama amerogwa, mdogo wangu Ally Kiba wacha kabisa kumuwekea Diamond kinyongo kwa ajili ya makosa yako mwenyewe, and you steel have time to correct your mistake na kuanza upya. Wacha kutumia mgongo wa mwenzako ili kusikika, umeona watu wako busy na Uno ya Harmonize sasa unaanza kutafuta attention ya watu kwa kutengeneza bifu zisizokuwa na kichwa wala mkia?! Shame on you, nikiwa kama baba mlezi wa waimbaji wote wa nyimbo za injili ambapo ndani yake yupo raisi wa shirikisho la muziki Tanzania ninakuonya uache hila zako mara moja. @officialalikiba @diamondplatnumz @rayvanny comment fupi fupi please sitaki povu kabisa MNIKOME.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 31, 2019
Simba SC yakwama kwenye machimbo ya almasi

Comments

comments