Timu ya Mbeya City FC kesho asubuhi itaondoka mjini Mbeya kwenda Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ziara ya michezo ya kirafiki.

Meneja wa Mbeya City, Geoffrey Katepa amesema, kikosi cha timu hiyo kitakuwa huko kwa michezo mitatu ya kujipima nguvu hadi juma lijalo.

Katepa, kiungo wa zamani wa Yanga alisema kwamba ziara inakuja baada ya mapumziko ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.

“Imekuwa ni taarifa njema kupatikana kwa michezo hii ya kirafiki na tutaitumia  kujiweka sawa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa Januari 17 dhidi ya Azam FC kule Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam,” alisema Katepa.

Katepa aliyewahi pia kuchezea Tukuyu Stars ya Mbeya, alisema kwamba Mbeya City itacheza mechi tatu kuanzia Ijumaa ya leo Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kabla ya kurejea Mbeya Jumatatu kuendelea na maandalizi ya mechi dhidi ya Azam.

Alisema mechi zote zitachezwa Uwanja wa Mandela na kwa mujibu wa ratiba wataanza na Magogo FC kabla ya kucheza na timu nyingine watakazopangiwa na wenyeji wao. Alisema watasafiri na kikosi cha wachezaji  25 na viongozi watano.

Lowassa atajwa sababu ya deni la Milioni 1 mbele ya Mkuu wa Mkoa
Jerry Muro Ajutia Makosa, Aomba Msamaha Wa Rais