Kamati ya rufaa ya maadili ya shirikisho la soka nchini TFF, kesho inatarajia kusikiliza rufaa ya Michael Richard Wambura ambaye alifungiwa kujihusisha na soka maisha, baada ya kukutwa na makosa ya matatu ya kinyume cha maadili ya Shirikisho hilo.

Kamati ya rufaa ya maadili itaanza kusikiliza rufaa hiyo, majira ya saa 5:00 asubuhi katika ofisi za Shirikisho la soka nchini TFF zilizopo Karume, Ilala jijini Dar es salaam

Wakili Emmanuel Muga anayemtetea Wambura, amethibitisha kupokea barua ya kufika mbeleya kamati hiyo, na imemtaka Wambura aende na utetezi wa maandishi ama njia ya mdomo ili kukamilisha usikilizwaji wa rufaa yake.

Wambura aliadhibiwa kifungo cha maisha kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) (c) cha Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la 2013 baada ya kupatikana na kosa la kupokea fedha za Shirikisho malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya Shirikisho.

Nape: Bila kuvumiliana kisiasa Tanzania itakuwa nchi ya hovyo
Video: Urusi yajaribu kombora linalofika kona zote za dunia

Comments

comments