Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema siku chache kabla ya Mbowe kushambuliwa, katika mitandao ya Kijamii kulisambaa video ya mtu anayejiita Mchungaji wa Kitaifa, Mchungaji Mashimo akisema “Kuna tukio litatokea mbele kwa Kiongozi wa Upinzani kushambuliwa” na kati ya majina aliyoyataja, jina Freeman Mbowe lilikuwepo.

Ametoa wito kwa Polisi wamkamate ili aleze hizo kauli zake huku akiwataka Polisi wanapofanya uchunguzi hawapaswi kufunga milango ya uchunguzi na kuliita hili ni tukio la kawaida kwasababu viashiria vinaonesha tukio hili lina muelekeo wa kisiasa.

Kauli ya Mnyika inakuja baada ya Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muroto kusema wanafanyia uchunguzi tukio la Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kushambuliwa na kuvunjwa mguu huku akipiga marufuku watu kulitumia kisiasa.

Mnyika amesema kati ya watu waliokuwa wanamshambulia Mbowe wapo waliosikika wakisema “Wewe unaisumbua sana Serikali, tunakushughulikia tuone kampeni utafanyaje.” Ametoa wito kwa Polisi na vyombo vya Usalama kuchunguza tukio hilo kwa mapana ili waliohusika wachukuliwe hatua.

Brazil yajitoa kombe la dunia
Floyd kuzikwa leo pembeni ya mama yake, Mshukiwa mkuu kifo chake apata dhamana