Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, Meek Mill ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha jela kwa miezi mitano.

Meek Mill aameachiwa jana kufuatia amri ya Mahakama Kuu ya mjini Philadelphia kutokana na hukumu yake hiyo kuonekana kuwa na utata mkubwa ndani yake.

Meek alihukumiwa kifungo cha miaka 2-4 jela na tayari alikuwa ameshatumikia kifungo cha miezi mitano jela.

Katika ukurasa wa wake wa Instagram Meek Mill ameandika

”Namshukuru Mungu, Familia yangu, Rafiki zangu, Team nzima ya Roc Nation akiwemo Jay Z, Zizia Perez na rafiki yangu Michael Rabin na mashabiki ”.

Mastaa wengi duniani akiwemo Jay Z na wengine wameonekana kufurahisha kuachiwa kwa msanii mwenzao.

Baadhi ya wasanii wa Marekani walioguswa na kuachiwa kwake ni Jay-Z, Kevin Hart, Fabolous, T.I na wengine.

7 mbaroni kwa tuhuma za uhalifu
Hii si Ndege ya kwanza kutua nchini- Mlinga

Comments

comments