Meek Mill ameamua kutangaza amani dhidi ya rapa Drake aliyekuwa hasimu wake wa muda mrefu, wakirushiana makombora kwenye nyimbo zao.

Ikiwa ni wiki kadhaa tangu Meek aachiwe huru, amesema kuwa kazi ya pamoja kati yake na Drake ni kitu ambacho kinawezekana tofauti na ilivyokuwa awali.

Harufu nzuri ya amani kati ya wakali hawa wa michano ilianza baada ya Drake kujiunga na kampeni ya kushinikiza Meek aachiwe huru iliyopewa hashtag ‘FreeMeek’, na ikafanikiwa.

Akifanya mahojiano na Angie Martinez, Meek alisema kuwa anaamini hivi sasa Drake hana chuki dhidi yake na kwamba hata yeye hana chuki dhidi ya rapa huyo.

‘Inawezekana tukafanya wimbo wa pamoja. Mimi sina chuki dhidi yake na naamini hata yeye hana chuki dhidi yangu. Nilipokuwa kwenye wakati ule [jela], niliona kwenye vyombo vya habari… alisema ‘muachieni Meek Mill (Free Meek Mill)’. Huo ulikuwa wakati mgumu kwangu ambao sikuwa na chochote kinachoendelea kuhusu muziki,” alisema Meek.

Aliongeza kuwa kabla wawili hao hawajaanza kuwa na uhasama kupitia muziki, walikuwa wanafahamiana katika maisha ya kawaida na kwamba Drake alikuwa anamsaidia pia.

Drake na Meek Mill 2014-2015

Meek alisema kuwa bado hajapata nafasi ya kuongea na Drake, lakini anaamini wakikutana wataongea na anaamini kilichotokea kati yao kilishapita.

Drake na Meek walikuwa na uhasama wa kurushiana maneno kwenye muziki, kila mmoja akiachia kombora maalum la kumshambulia mwenzake (dis track) na kujibiwa vikali na mwenzake.

 

Wachungaji wanusurika kipigo baada ya kushindwa kumfufua mfu
Video: JPM atoa maagizo 5 mazito mafuta ya kula, Wachungaji wanusurika kichapo baada ya kushindwa kumfufua mfu

Comments

comments