Mfanyabiashara wa nguo za mitumba jijini Dar es Salaam, Hadija Hassan amefungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akimlalamikia Ali Saleh Kiba, maafuru kama Ali Kiba kwa kutotoa matunzo ya mtoto aliyezaa naye.

Kupitia hati ya Mashtaka, mlalamikaji amedai kuwa alijifungua mtoto huyo aliyezaa na Ali Kiba mwaka 2013 katika hospitali ya Mikocheni jijini Dar es Salaam na kwamba hadi sasa mtoto huyo hapati matunzo muhimu kutoka kwa baba yake.

Hadija anaiomba Mahakama kuamuru Ali Kiba awe analipa kiasi cha sh 1.41 milioni kwa mujibu wa sheria, akirejea sheria ya watoto ya mwaka 2009.

Akielezea mgawanyo wa kiwango hicho cha fedha, alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, “Ali Kiba anapaswa kutoa huduma kila mwezi, chakula sh 150,000, matunda sh 50,000, chakula cha ziada sh. 50,000, michezo na burudani za watoto sh. 100,000, nguo sh. 60,000 na matibabu shilingi 50,000.”

Alisema mbali na huduma hizo tajwa zinazopaswa kutolewa kila mwezi, anaiomba mahakama hiyo kumuamuru mlalamikiwa kutoa sh 950,000 kama ada shule kwa muhula mmoja.

Hadija amefungua kesi hiyo akisaidiwa na Kituo cha Wanawake cha Msaada wa Kisheria (WLAC).

Mlalamikiwa anayetakiwa kujitetea, alifunga ndoa hivi karibuni na mrembo kutoka Kenya na harusi yake ilivuta usikivu wa Afrika Mashariki hususan Kenya na Tanzania kutokana na ukubwa wa jina lake.

Yanga yaburuza mkia baada ya kuchezea kichapo
Video: Ali Kiba kortini matunzo ya mtoto, Waumini 'wampiga' mawe Askofu KKKT

Comments

comments