Watuhumiwa watano wanaokabiliwa na shtaka ya kuhujumu uchumi akiwemo mtuhumiwa namba moja Mohamed Mustapha wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na makosa 199 ikiwemo kugushi nyaraka.

Mawakili  wa serikali kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa , Leornad Swai na wenzake  wakisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Huruma Shaidi inadaiwa kuwa washtakiwa hao wakiongozwa na Mohamed Mustapha wameisababishia serikali hasara ya bilioni 15.

Pamoja na hayo wakili  upande wa washtakiwa Harisson Lusiepo  amekiri ni kweli wateja wake wameonekana kuwa na makosa mengi huku Mustapha Mohamed ameonekana kuwa na makosa mengi .

Mohamedi Mustapha anakabiliwa na Shtaka la kugushi nyaraka za makampuni mbali mbali ili kujipatia fedha kinyume cha sheria na inasemekana ndiye Mtuhumiwa wa kuchukua milioni 7 kwa dakika

Hata hivyo kutokana na uzito wa makosa hayo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu au kuongea chochote mbele ya mahakama hiyo, Pia wamerudishwa tena rumande huku kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa julai 25 .

 

TFF Yasaka Mkurugenzi Wa Masoko
Cheka: Eric Omondi azua balaa akimuiga Museveni kuweka kiti barabarani kuongea na simu