Jeshi la Polisi nchini limeendelea kufanya msako mkali kwa lengo la kumtafuta Bilionea, Mohammed Dewji ambaye alitekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam.

Jeshi hilo limeimarisha ulinzi na kuendelea kufanya msako katika Pwani ya Bahari ya Hindi jijini humo, wakimulika zaidi Hotel zilizoko eneo hilo.

Meneja Mkuu wa Yatch Club, moja kati ya hotel kubwa katika eneo la Pwani ya Bahari ya Hindi, amekaririwa na Mwananchi akieleza kuwa jeshi la Polisi limekuwa likichunguza picha za CCTV Camera za hotel hiyo na kuimarisha ulinzi.

Watu kadhaa wanashikiliwa na jeshi hilo kutokana na tukio hilo la utekaji lililotokea majira ya saa 11 alfajiri, katika hoteli ya Colosseum ambapo Bilionea huyo alienda kufanya mazoezi.

Kati ya waliokamatwa na jeshi hilo ni pamoja na msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara aliyedaiwa kusambaza habari hizo kinyume cha taratibu na uhalisia wa chanzo alichodai kimemtuma ambacho ni familia ya Mo.

Mo anamiliki asilimia 49 ya hisa za Klabu ya Simba na ametajwa kwenye jarida la Forbes kama bilionea kijana akiwa na utajiri wa $1.5 bilioni.

Video: Rais Magufuli, Mkewe wamtembelea Mama Maria Nyerere
Bomba la mafuta laua watu 30

Comments

comments