Mtoto wa miezi 11, Sabra Chanzo aliyenusurika kwenye ajali iliyotokea usiku wa kuamkia jana eneo la Dundani, Mkuranga mkoa wa Pwani amelazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili MOI baada ya kuvunjika miguu yote miwili.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Moi, Almas Jumaa amesema walimpokea jana na anaendelea kupatiwa matibabu.

Amesema amevunjika miguu yote miwili na yupo na bibi yake akiendelea kuhudumiwa.

”Yupo na bibi yake anaendela kutibiwa hali yake siyo mbaya amevunjika miguu yote miwili, inawezekana wazazi wake wote wamefariki kwenye ajali.

Watu 14 wakiwemo sita wa familia moja baba, mama na watoto wao wanne walifariki usiku wa kuamkia jana eneo la Dundani Wilayani Mkuranga, Pwani.

Teknolojia ya VAR yamkera Nordin Amrabat
Granit Xhana, Xherdan Shaqir waachwa huru